Dr John Magufuli (@MagufuliJP )

Dr John MagufuliBio The Fifth President of The United Republic of Tanzania.
Location Tanzania
Tweets 200
Followers 505,7K
Following 9
Account created 16-07-2015 04:46:06
ID 3378377920


Twitter Lite : Vijana wangu - TAIFA STARS🇹🇿
Muda mfupi ujao nitakuwa nikitazama mchezo kati yenu na Timu ya Taifa ya Lesotho 🇱🇸.
Mimi na Watanzania wenzangu tunawatakia mchezo mwema, mrudi na ushindi.

Twitter Lite : Nawashukuru wote mlionitakia heri katika siku yangu ya kuzaliwa. Mungu ni mwema.
Nimepokea salamu nyingi japo sikuweza kuwajibu wote, lakini muamini kuwa nimezipata. Nawaomba Watanzania tuendelee kudumisha amani,upendo,mshikamano na tuchape kazi za kulijenga Taifa letu.

Twitter Lite : Nakupa pole Mhe. Rais Museveni na wananchi wote wa Uganda kwa kuwapoteza watu zaidi ya 40 katika ajali ya maporomoko ya udongo iliyotokea katika Wilayani Bududa. Watanzania tunaungana nanyi katika kipindi hiki cha majonzi na tunawaombea majeruhi wote wapone haraka Yoweri K Museveni

Twitter Lite : Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya ajali ya basi iliyotokea Kericho nchini Kenya na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 50. Nakupa pole Mhe. Rais Uhuru Kenyatta, familia za marehemu na Wakenya wote. Mungu aziweke roho za marehemu mahali pema na majeruhi wapone haraka. Uhuru Kenyatta

Twitter Lite : Nakupongeza Mhe. Rais Yoweri Museveni na wananchi wote wa Uganda kwa kuadhimisha miaka 56 ya Uhuru. Kwa niaba ya Watanzania nawaahidi kuundeleza na kuukuza uhusiano na ushirikiano wetu wa kihistoria. Kwa pamoja tudumishe ujirani mwema, udugu na urafiki kwa manufaa yetu sote.

Twitter Lite : Cde. Mnangagwa. On behalf of the Government and people of Tanzania,I convey my sincere congratulations on your victory in the Presidential Election of Zimbabwe.Your victory is a reflection of the confidence reposed in you by the people of Zimbabwe in leading them to prosperity.

Twitter Lite : MAN OF GOD, Rev. TB JOSHUA
On behalf of my family, I extend my heartfelt wishes on your 55th Birthday. May the Almighty God bestow upon you exceeding divine inspiration so that you can bring deliverance to more people and spread his fragrance across nations. HAPPY BIRTHDAY TO YOU

Twitter Lite : Nimesikitishwa na kifo cha Maria na Consolata. Nilipokwenda hospitali waliliombea Taifa. Walikuwa na ndoto ya kulitumikia Taifa. Poleni familia, Masista wa Maria Consolata na wote walioguswa, pumzikeni mahali pema wanangu. BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.

Twitter Lite : Ninayo furaha kukupongeza Mzee wangu Alhaji Ali Hassan Mwinyi kwa kutimiza miaka 93. Busara zako, ushauri, upendo, unyenyekevu, ucha Mungu na ushirikiano kwa Watanzania ni jambo tunalojivunia sana. Nakutakia afya njema na maisha marefu yenye furaha na amani. HAPPY BIRTHDAY.

Twitter Lite : Marehem Sokoine hatasahaulika katika historia ya Tanzania, ni wito wangu kwa watanzania tumuige na kumuishi. Ni rai yangu pia tumuenzi kwa kujenga umoja wetu , kupiga vita rushwa na kuchapa kazi . Mungu aiweke roho ya marehemu Edward Moringe Sokoine mahala pema peponi 3/3

Twitter Lite : Wakati tunapoazimisha siku kama hii ya kifo chake, watanzania tuige mfano wake kwani alikuwa msema kweli, asiyeogopa, mpiga vita rushwa,ufisadi, unyonyaji,mzalendo wa kweli na aliyechukia rasilimali za watanzania kuibwa 2/3

Twitter Lite : Katika siku kama ya leo tarehe 12 Aprili 1984 nikiwa Mpwapwa JKT nikitumikia jeshi langu “Oparesheni Nguvukazi” tukatangaziwa kifo cha marehem Edward Moringe Sokoine, ilikuwa siku ya majonzi shujaa huyu niliyemjua na kumshabikia ikawa siku yake ya mwisho 1/3

Twitter Lite : I have learnt with deep sorrow the sad news of the demise of Winnie Mandela, a woman of an exceptional courage and strength.
She will always be remembered for the important role she played during the struggle against apartheid.
May the Almighty God rest her soul in eternal peace.

Twitter Lite : Im very glad that we have commenced the second lot of our central line standard gauge railway construction from Morogoro to Dodoma. As we celebrate this important milestone in our countrys development lets steadfastly preserve our peace, unity and solidality.

Twitter Lite : Nawapongeza wanawake wote kwa kusherehekea siku yenu ya leo na hasa kwa mchango wenu mkubwa mnaoutoa kwa jamii. Daima tutaendelea kuwaheshimu, kuwapa ushirikiano na kutambua juhudi zenu katika kujenga ustawi wa jamii yetu.

Twitter Lite : Nimesikitishwa sana na kifo cha mwanafunzi Akwilina Akwilini wa Chuo cha Usafirishaji (NIT).Natoa pole kwa familia,ndugu,wanafunzi wa NIT na wote walioguswa na msiba huu.Nimeviagiza vyombo vya dola kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua za kisheria waliosababisha tukio hili.

Twitter Lite : My heartfelt condolences to Morgan Tsvangirai’s family. Our thoughts and prayers are with the Zimbabwean people during this time of grief and inexpressible sorrow.

Twitter Lite : Nawapongeza viongozi, wanachama na wapenzi wote wa CCM kwa kutimiza miaka 41. Tunaposherehekea mafanikio yetu tuendelee kutunza Amani na umoja wetu, tuchape kazi kwa maslahi ya nchi yetu na Serikali inayoongozwa na CCM.